25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Jenista aipongeza Bodi ya NSSF

Na MWANDISHI WETU -MOROGORO 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, ameipongeza Bodi ya Wadhamini na Menejimenti ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kufanya mambo mengi mazuri kwa muda mfupi.

Jenista, alisema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akifungua mkutano wa baraza la 45 la wafanyakazi wa NSSF lililofanyika mkoani Morogoro.

Alisema bodi ya wadhamini na menejimenti, imeboresha uendeshaji wa shirika kwa kujiunga na mifumo ya kielektroniki kama mfumo wa malipo ya Serikali wa kielektroniki (GePG), ambao waajiri wanautumia kuwasilisha michango NSSF na mfumo wa kielektroniki wa uhasibu (Orcale Financial System) ambayo imeboresha utendaji wa Shirika katika kipindi kifupi.

Jenista, alisema faida za mifumo hiyo, ni kusaidia kupunguza malalamimo ya wanachama ikiwemo ya kupata malipo yao kwa wakati.

Alisisitiza uwajibikaji kwa watendaji wa shirika hilo kwa kutumia mabaraza hayo kwa sababu yapo kisheria.

 â€œMenejimenti, mheshimiwa mwenyekiti wa bodi (Balozi Ali Idi Siwa) mmenifariji sana. Nimeona mmetengeneza mfumo wa kielektroniki wa kihasibu, hongereni mmefanya kazi nzuri,” alisema Jenista. 

Aliitaka menejimenti kuongeza nguvu katika kuandikisha wanachama kwa sababu sekta binafsi ina wanachama wengi wanaotakiwa wajiunge katika shirika hilo.

Alisema hatavumilia kwa mtendaji yeyote ambaye hatafikia malengo waliyojiwekea katika shirika hilo.

Alisisitiza kampuni binafsi kujiunga na NSSF, kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria ya mwaka 2018.

Aliwataka wafanyakazi kuacha kukaa ofisini, badala yake waende kuandikisha wanachama wapya.

Aliagiza wastaafu wasisumbuliwe wanapofuatilia mafao yao na wahudumiwe haraka kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Aliagiza kutumia Baraza la Wafanyakazi kupima utendaji wa watumishi wa shirika hilo na wale walioshindwa kutimiza malengo wachukuliwe hatua.

Alisema kazi kubwa ni kuhakikisha kila Mtanzania katika sekta binafsi na isiyokuwa rasmi, anaandikishwa kwa mujibu sheria ya hifadhi ya jamii, hivyo NSSF ihakikishe inaandikisha wanachama wapya wengi kadiri iwezekanavyo. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Balozi Siwa, alisema mwaka wa fedha wa 2018/19, shirika lilijiwekea lengo la kuandikisha wanachama wapya 119,749, ambapo hadi kufikia Machi, mwaka huu, ambayo ni robo tatu ya mwaka, wameandikisha wanachama 98,969 sawa na asilimia zaidi ya 82.

Pia shirika lilikusanya Sh bilioni 594.94 kutoka kwa wanachama wake, ikiwa ni asilimia 104.38 ya lengo la kukusanya kiasi cha Sh bilioni 570.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles