26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

‘Jamii ipewe elimu kuhusu bayoanuai’

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Ukosefu wa uelewa mpana kuhusiana na viumbe hai au Bayoanuai ni moja ya sababu inayochangia jamii kushindwa kutunza mazingira.

Hatua hiyo pia inachochea kushindwa kutathimini kwa kina mchango unaotokana na bayoanuai katika pato la taifa.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo Mei 17, na Dk. Elikana Kalumanga ambaye ni Meneja Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili katika mjadala wakuwajengea uwezo wanahabari kuhusu bayoanuai.

Dk. Elikana Kalumanga ambaye ni Meneja Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili.

Kwa mujibu wa Dk. Kalumanga, bayoanuai ni pamoja na aina milioni 8 ya mimea na wanyama wanaopatikana kwenye sayari, mifumo ya ekolojia inayotumika kama makazi yake, na utofauti wa kimaumbile.

“Ni la zima tukiri kwamba bado jamii yetu haina ufahamu wa kutosha kuhusu bayoanuai licha ya ukweli kuwa ndivyo vitu vinavyotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku na kufanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi.

“Mfano, kuna vitu kama bahari, maziwa, mito, mabonde mfano hapa Dar es Salaam tunafurahia kuona tunapata hewa nzuri na maji ya kunywa bila kuzingatia kuwa kuna sehemu yanatoka.

“Ukija katika eneo la misitu mfano miombo, mikoko na aina nyingine ambayo hii inachochea sana uwepo wa bayoanuai lakini kutokana na jamii yetu kutokuwa na ufahamu wa kutosha imekuwa ikiikata ovyo,” amesema Dk. Kalumanga.

Dk, Kalumanga amesema kuwa hadi sasa kama nchi bado hatujapata mchango halisi wa bayoanuai katika pato la taifa.

“Ukiangalia upande wa misitu inachangia asilimia 3.5 tu katika pato la taifa, hivyo utabaini kwamba hadi le bado hatujapata mchango halisi wa bayoanuai kwenye pato letu la taifa,” amesema Dk. Kalumanga na kusisitiza kuwa:

“Vyombo vya habari mna kazi kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii, mtu ajue kwamba kumwe misitu mbali na kupata mbao tu kuna faida nyingine inayopatikana, au maji siyo kutupa samaki tu kumbe kuna faida nyingine,” amesema.

John Noronha ambaye ni Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili.

Akitoa mada katika mjadala huo, John Noronha ambaye ni Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, RTI, Mshirika mtekelezaji wa USAID inayotekeleza Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili amesema maeneo ya bayoanuai na uhifadhi ni nyenzo muhimu na yana mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Yanachukua karibu asilimia 37 ya hewa chafu inayozalishwa duniani, hivyo kuendelea kufanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi, hata hivyo bado kuna changamoto ukiangalia mfano Dar es Salaam ukiangalia sehemu nyingine ya miti imekatwa.

“Kadri miundombinu inavyoongezeka ndivyo miti inavyozidi kuisha bila kuja na mbinu mbadala jambo ambalo utaona kwamba linaathiri uhifadhi kwa ujumla. Hivyo, Bayoanuai ni nguzo inayofanya sayari yetu kuwa mahali pazuri pa kuishi. Bayoanuai huathiri vipengele vyote vya maisha ya binadamu, hutupa hewa safi na maji safi, hutupa lishe bora, hutupa uelewa wa kisayansi na dawa.

“Pia huwezesha miili yetu kukabiliana na magonjwa na hukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kubadilisha au kuondoa kipengele chochote kwenye utando huo huathiri mfumo mzima wa maisha na kunaweza kusababisha madhara mabaya. Bila mazingira, hatuwezi kuishi duniani,” amesema Noronha.

Anna Lauwo ambaye ni Mkuu wa sehemu ya utangazaji utalii ikolojia – Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

Upande wake, Anna Lauwo ambaye ni Mkuu wa sehemu ya utangazaji utalii ikolojia – Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), amesema athari wa mabadiliko ya tabianchi zimenza kuonekana tangu mwaka 1976 huku kwa Tanzania ikianza mwaka 2009.

“Kwa upande wa Tanzania mwaka 2009 ndiyo ilijua kuwa tunaweza kupata madhara ya mabadiliko ya tabianchi na mradi wa kwanza ulikuwa Babati mkoani Singida ambao ulikuwa ukihifadhi miti na kulima matunda maji, yaani mvua ikinyesha maji yanaingia chini kisha yanahifadhiwa na miradi mingine yote hiyo ikiwa ni katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

“Kwa hiyo hizo shughuli zimeendelea hivyo huku Serikali ikiendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu changamoto hii, mwaka 2014 baada ya Mkutano wa Ujerumani ikaamuliwa kwamba ili dunia iweze kurejesha uonto wake wa asili ekta milioni 350 wakakubalina kugawana kila bara ambapo Afrika ilikubali kurejesha hekta milioni 100.

“Baadae Afrika ikakaa katika kikao kilichofanyika Afrika Kusini mwaka 2014 ambapo kila nchi ilitakiwa kueleza itachangia kiwango gani kulingana na uchafuzi, ambapo TFS ilichaguliwa kuwa mratibu na ikaonekana kwamba uharibifu wa mazingira kwa Tanzania ilikuwa ni 400,960 ambapo Tanzania ilisema inachangia hekta bilioni 5.2 ambapo hii inagusa maeneo na sekta mbalimbali katika kuhakikisha dunia inakuwa salama kwakuzuia athari za mabadiliko,” amesema Lauwo na kuongeza kuwa Serikali haliwezi kukwepa eneo hilo na lazima ifanye mbinu sana za kuelimisha watu namna ya kudhibiti athari za mazingira ikiwamo kupanda misitu kama inavyohimiza TFS.

Mmoja wa washiriki wa mjadara huo, Bakari Kimwanga amesema mjadala huo umekuwa na mchango mkubwa kumjengea uwezo kuhusu bayoanuai nakwamba jamii zikiwamo mamlaka zinapaswa kuhimizwa kuhusu umuhimu wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles