24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Ileje kuruka na wanonyemelea fedha za BOOST

Na Denis Sikonde, Songwe

MKUU wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi amewataka wasimamizi wa miradi ya Boost kuwa na uchungu na fedha zilizotolewa na Serikali ili zitumike kwa lengo lililokusudiwa.  

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikumbilo kata ya Chitete wilayani humo mapema leo Mei 16, 2023 wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boost katika zoezi la uchimbaji wa msingi kwenye eneo inapojengwa shule mpya kwenye kijiji hicho.

Mgomi amewataka wasimzmizi wa mradi huo ikiwemo kamati ya Boost wilaya kuweka uwazi kwenye miradi hiyo ambapo serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni moja.

Mgomi amesema wananchi wanatakiwa kuwa wa kwanza kulinda mradi huo kwa kuripoti kwenye vyombo husika pindi watakapobaini watu wanaojaribu kuiba hata mfuko mmoja wa saruji au nondo ili wawajibishwe.

“Kazi ya mradi wa Boost utekelezwe ipasavyo ole wako ubainike unanymelea fedha hizo nawahakikishieni tutaruka wote juu kwa juu ili wote wanaokwamisha miradi iwe mwisho kwa wilaya Ileje,” amesema Mgomi.

Aidha, Mgomi amewataka wananchi kwenye maeneo yaliyonufaika na mradi huu washirikiane washiriki kwa karibu sana ili takwa la serikali ya awamu ya sita litimie kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi na walimu kwenye maeneo hayo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje, Hermani Njeje amesema nguvu ya wananchi inatakiwa ithaminiwe kwenye mradi huo kwani nguvu yao ithaminiwe ili fedha itakayookolewa itumike kuongeza miundombinu mingine kwenye shule hizo.

Upande wake Diwani wa kata hiyo, Osiwelo Kyomo amewasihi wananchi wa kata hiyo kuonyesha ushirikiano pindi wanapohitajika ili kumaliza kwa wakati huku akimsihi Mhandisi wa wilaya kutowaachia mafundi mradi mpaka itakapotokea changamoto akidai hali hiyo itapelekea miradi kutokamilika kwa wakati.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwamo, Frank Ndimbwa na Atanasi Masebo wameishukuru Serikali kwa kuwapa mradi huku wakiomba ushirikiano kwa wananchi wa kata hiyo kuhakikisha lengo la serkali la kupunguza msongaamano kwa wanafunzi wa shule mama ya Ikumbilo linatimia.

Ikumbukwe kuwa Wilaya Ileje imepokea fedha zaidi ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kujenga miundombinu ya madara kwenye shule nane wilayani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles