25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

IRENE UWOYA apotea mitandaoni

 JESSCA NANGAWE 

STAA wa filamu nchini, Irene Uwoya amesema kwa sasa hatumii mitandano ya kijamii baada ya akaunti yake ya Instagram kupata matatizo. 

Uwoya ambaye kwa sasa anaonekana kimya huku wengi wakidai amefulia amesema baada ya ile akaunti yake ya kwanza kupotea kutokana na kusahau pasward alitumia nyingine lakini akanyang’anywa na wahusika wa mtandao huo kwa madai si yakwake. 

Mrembo huyo amekiri kuwa pamoja na mitandao ya kijamii kuwa sehemu ya yeye kupata kipato kwa kutangaza bidhaa mbalimbali lakini amewaachia wahusika kushughulikia hilo na sasa haingii kabisa kwenye mitandao. 

“Nilipoteza namba ya siri ya akaunti yangu ya kwanza ambayo ilikua na watu zaidi ya milioni 4, nikabahatika kupata nyingine nayo nimenyang’anywa kwa madai si yangu, sina tatizo kwa kuwa maisha yangu yanakwenda kama kawaida ila kikubwa kwa sasa sipo kabisa huko,”alisema Uwoya. Hata hivyo alisema matukio mbalimbali anayohusishwa nayo amekua akiyapata kupitia watu wake wa karibu lakini hayamuumizi kwa kuwa si ya kweli. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles