IRAN YAISHTAKI MAREKANI

0
842

TEHRAN, IRAN


SERIKALI ya Iran jana iliwasilisha kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kupinga vikwazo vipya ilivyowekewa na Marekani.

Rais Donald Trump wa Marekani aliiwekea Iran   vikwazo vigumu wiki tatu zilizopita, licha ya vikwazo hivyo kuwahi kuondolewa baada ya  makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi zenye nguvu mwaka 2015.

Wanasheria wanaoiwakilisha Iran wameitaka ICJ kuiamuru Marekani kuondoa vikwazo hivyo.

Wanasheria wa upande wa Marekani wanatarajiwa kuwasilisha kesi yao mbele ya mahakama leo.

Trump aliyaeleza makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwamo Ujerumani, kuwa ni ya kushtusha na yanayoelemea upande mmoja.

Alisema makubaliano hayo  pia hayakufanikiwa kufikia lengo la msingi la kuzuia njia zote za kuiwezesha Iran kutengeneza bomu la nyuklia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here