27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

IDARA YA MAJI MBEYA YAPEWA ONYO

dawasco

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

SERIKALI mkoani Mbeya imezuia makato ya ankara ya maji yaliyokuwa yakikatwa kwa wananchi wa Mji mdogo wa Ipinda hadi pale mamlaka husika itakapofikisha huduma hiyo.

Uamuzi huo umetolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Ipinda wilayani hapa.

Alisema haiwezekani wananchi kukatwa fedha za malipo ya maji kwa mwezi wakati huduma hiyo haiwafikii kutokana na mabomba waliyowafungia kushindwa kutoa maji kwa kipindi kirefu.

“Jambo hili haliwezekani na Serikali haitawavumilia watu wachache ambao wanachangia kuyafanya maisha ya Watanzania kuwa magumu, kwani mamlaka ya maji imewezaje kutoza ankara za maji wakati huduma haipatikani,” alihoji Makalla.

Alisema kama maji hayatoki, idara imewezaje kusoma units na kutoza kama si kufanya kazi kwa mazoea, ni vema mhandisi akalishughulikia suala hili haraka iwezekanavyo.

“Mhandisi ni lazima ufuatilie suala hili kwenye mamlaka husika na kuhakikisha wananchi hawalipishwi fedha hadi huduma itakapowafikia na kwamba kuendelea kufanya hivyo ni kuwadhulumu wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali,” alisema.

Alisema Mji wa Ipindi unakua na watu wanaongezeka lakini huduma ya maji safi na salama bado ni changamoto.

Aidha, Diwani wa Kata ya Ipinda  ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Dk. Hunter Mwakifuna, alisema ukosefu wa maji katika eneo hilo ni changamoto kubwa ambayo inawakabili wananchi wake.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles