27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Temeke yafanikiwa kuondoa viungo vya uzazi vya kike kwa mgonjwa mwenye jinsia mbili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke jijini Dar es Salaam imefanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume.

Upasuaji huo umefaywa na jopo la madaktari kutoka hospitali hiyo, na limeongozwa na Daktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo, Dk Hussein Msuma pamoja na wasaidizi wake, Dk. Hamis Mbarouk, Curtius Mbalamula, Mkati na Sr Shani Maupa.

Hiyo ni kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo na kwa mara ya kwanza kwa hospitali za rufaa zilizopo Tanzania.

Kufanyika kwa upasuaji huu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temke ni moja ya mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya Tanzania kwani moja ya jitihada ya Serikali na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha hospitali zetu za Tanzania zinauwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi.

Aidha, huu ni muendelezo wa upasuaji Bingwa na Bingwa bobezi katika Hospitali hii, kwani hospitali pia ilifanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa saratani ya figo bila kutoa figo pamoja na kutoa jiwe katika figo.

Mafanikio haya yanatokana na uwepo wa madaktari bingwa na Bingwa bobezi wenye utaalamu katika fani mbalimbali za afya katika hospitali hii.

Akizungumza baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizo tolewa katika upasuaji, Dk. Hussen Msuma amesema kuwa ni kweli Mgonjwa alifika Hospitalini akiwa na muonekano wa jinsia ya kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili yaani umbile la kike na la kiume, hivyo kupelekea upasuaji huu.

“Upasuaji tumefanya kwa mgonjwa aliekuwa na Muonekano wa nje wa jinsia ya kiume ila alikua na mifumo ya uzazi ya jinsia mbili; ya kiume kwenye korodani ya kulia na yakike kwenye korodani ya kushito.

“Kwa lugha ya kitaalamu huu upasuaji unaitwa scrotal hystero-salpingo-oophorectomy na kwa lugha rahisi ni upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume.

“Ugonjwa huu unatokana na changamoto wa ukuaji wa kijinsia (ovotesticular DSD), ni ugonjwa nadra na adimu sana kutokea ambapo binaadamu huzaliwa na viungo vya ndani vya uzazi (gonadi) za jinsia zote (ovari za kike na korodani za kiume),” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles