23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

HECHE: NATISHIWA MAISHA

Na Esther Mbusi, Dodoma


MBUNGE wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), amesema amepokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana ikiwa ni siku chache baada ya kuchangia bungeni taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Katika mchango wake, Heche alizungumzia namna Serikali ilivyoudanganya umma kupitia mradi wake wa Pasipoti Mtandao (E-Passport) na kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa, maelezo ambayo alidai yametokana na taarifa ya Kamati ya PAC.

Hata hivyo, Heche alishindwa kusema amekwishatoa taarifa ripoti polisi au.

“Taifa letu linapitia wakati ngumu, genge la wahalifu wa kiuchumi na kisiasa kamwe lisitarajie nitatishika ama kubadili msimamo. Vitisho vilivyoanza dhidi yangu baada ya kuibua ufisadi huu havitaniogopesha kamwe.

“Njia zao ovu ama kunitisha kutaka kuchafua heshima yangu au kunitengenezea kesi au kunifanyia alichofanyiwa Tundu Lissu hazitanirudisha nyuma,” alisema Heche.

Hata hivyo, akizungumza na MTANZANIA mjini Dodoma jana, Heche alisema anakamilisha baadhi ya nyaraka muhimu ili apeleke bungeni kuomba iundwe kamati teule ya kibunge itakayochunguza ubadhirifu aliouibua.

Alisema anahitaji mambo mawili, kwamba serikali ionyeshe kuwa ilitoa kazi ya e-passports kwa zabuni na washindani walikuwa kina nani.

“Mbili, serikali iweke wazi nyongeza ya mkataba ya vitambulisho vya taifa na ieleze sababu za gharama ya kutengeneza kitambulisho kupanda kutoka Sh 17,000 kwa kitambulisho hadi Sh 26,000 kwa kitambulisho.

“Serikali itambue kuwa rasimu ya taarifa ya PAC iliyonyofoa taarifa kuhusu NIDA (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) tunayo na tunajua njama zilizotumika kuondoa eneo hilo.

“Hata nikiuawa Watanzania watajua ukweli kwani taarifa hiyo ipo kwa wabunge wengi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles