HakiElimu yatoa msaada wa vitabu halmashauri tatu Simiyu

0
1447

Derrick Milton, SimiyuTaasisi ya HakiElimu Tanzania, imetoa msaada wa vitabu zaidi ya 600 vya ziada kwa shule za msingi, sekondari na kidato cha sita katika Halmashauri za Bariadi Mji, Bariadi Vijijini pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu.

Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwa Kaimu Ofisa Elimu wa  Sekondari Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Peter Mosha, Mratibu wa taasisi hiyo Wilaya za Bariadi Mji, Bariadi vijijini na Itilima Janeth Kato kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu nchini Dk. John Kalaghe, leo Jumanne Oktoba 16.

Amesema lengo ni kuboresha usomaji kwa wanafunzi, taaluma pamoja na kuongeza mwamko wa wananchi katika kupenda elimu.

“Vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi, walimu huku kwa ajili ya wananchi kwa ujumla kujisomea katika kuongeza mwamko wa kupenda elimu,” amesema Mosha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here