22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Gwajima ateta na JPM, amtaka kutorudi nyuma Stigler’s Gorge

Na NORA DAMIAN

-DAR ES SALAAM

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa juhudi zake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ukiwemo wa kuzalishaumemekwa kutumia maporomoko ya majiya Mto Rufiji- Stigler’s Gorge, akisema wanaoupinga wanaendeleza siasa za kimataifa.

Alitoa pongezi hizo jana alipokutana na Rais Magufuli Ikulu na kusema kupitia mradi huo utazalishwa umeme mwingi kuliko uliowahi kuzalishwa hapa nchini.

 “Kwanza ni jambo zuri kuelewa kwamba ili ule chipsi mayai lazima uvunje baadhi ya mayai, kuna mayai lazima yavunjike ili upate chipsi mayai.

 “Namshukuru sana Rais kwa juhudi zake, hasa za Stigler’s Gorge, mahali ambapo tutazalisha umeme mwingi kuliko tuliowahi kuzalisha hapo zamani. 

“Tukumbuke wakati wa Mwalimu (Julius) Nyerere, (Ali Hassan) Mwinyi, (Benjamin) Mkapa na (Jakaya) Kikwete tulizalisha umeme kiasi, lakini kupitia mradi huu tutazalisha umeme mwingi kuliko Tanzania ilipoanza,” alisema Askofu Gwajima.

Alisema watu waliokuwa wanapinga mradi huo ni wale wanaoendeleza siasa za kimataifa na kushauri Serikali iendelee kusimamia msimamo wake.  

“Watu wengi wa Magharibi wanasema eneo hilo ni kwa ajili ya mazingira na mambo mengine, lakini ni siasa tu za kimataifa, ukiangalia miaka iliyopita kulikuwa na mkataba Japan wa Kiota, Marekani ilikataa kuusaini kwa sababu ikipunguza viwanda itaua nchi yake. Hata sisi pia tunatakiwa tulinde ‘interest’ (masilahi) zetu,” alisema.

Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Rufiji unaotekelezwa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) unagharimu Sh trilioni 6.6.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu na nusu, unatekelezwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Ubia ya Arab Contractors (Osman A. Osman Co) na Elsewedy Electric zote za nchini Misri zinazojenga bwawa litakalotumika kufua megawati 2,115 za umeme.

Rais Magufuli alisema walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huo kwa sababu Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji umeme kama vile maji, gesi asilia, upepo, joto ardhi, makaa ya mawe na madini ya urani. 

Alisema walifikia uamuzi huo kwa kuangalia vigezo vikubwa vine, ambavyo ni uhakika wa chanzo, gharama za utekelezaji, uzalishaji wa umeme, tija au manufaa yanayotarajiwa na kugundua kuwa mradi wa maji ya Rufiji ndio unafaa zaidi kwa sababu chanzo chake ni cha uhakika na maji yake yanatoka katika mito inayotoa wastani wa mvua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles