29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

GUCCI AMNYIMA MAMA YAKE MWALIKO WA HARUSI

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Radric Davis ‘Gucci Mane’, ametupiwa lawama na familia yake baada ya kumnyima kadi ya mwaliko mama na kaka yake.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 37, wiki iliyopita alifunga ndoa na mpenzi wake Keyshia Ka’oir, hivyo aliamua kufanya sherehe yenye thamani ya dola milioni 2, ambazo ni zaidi ya bilioni 4 za Kitanzania.

Katika sherehe hiyo, Gucci Mane hakuweza kumpa mwaliko mama yake wala kaka yake, lakini aliwapa rafiki zake wa karibu kama vile rapa Rick Rose, P.Diddy na wengine wengi.

Kitendo hicho kimeacha maswali mengi ambayo hayana majibu, huku familia yake ikibaki kwenye mshangao mkubwa.

“Ukweli ni kwamba mimi na mama hatukupewa mwaliko wa kwenda kwenye sherehe hiyo, tumeshangaa sana na hatujui ni kwanini, tunajisikia vibaya sana, nilitakiwa kuwepo nikiwa kama kaka na mama pia alitakiwa kuwepo, lakini nadhani yeye ana furaha moyoni mwake,” alisema kaka wa msanii huyo Nate.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles