33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

GGML yang’ara tuzo za PRST, yanyakua tuzo 2

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeendelea kufanya vyema kwenye nyanja mbalimbali zinazogusa jamii na serikali kwa ujumla baada ya Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Stephen Mhando kuibuka mshindi wa Tuzo ya Afisa Uhusiano Bora kwa mwaka 2022 kwenye sekta ya madini.

Tuzo hizo za umahiri zilitolewa Februari 18, 2023 jijini Dar es Salaam na Chama cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST).

Mbali na Mhando, GGML pia iliibuka mshindi wa pili katika tuzo ya taasisi bora Inayowajibikaji kwa Jamii (CSR). Tuzo hizo kwa pamoja zilipokewa na Mhando.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mhando aliwashukuru wadau mbalimbali ikiwamo wale anaofanya nao kazi hasa ikizingatiwa kwa asilimia kubwa ndio wamemuwezesha kuibuka mshindi na kuwa kati ya maofisa uhusiano nguli nchini kwenye sekta ya madini.

Tuzo hizo ambazo zimetolewa kwa mara ya kwanza na PRST, zinalenga kukuza na kuhamasisha ubora wa kitaaluma, ubunifu katika kupanga, kutetea, kushawishi, kutekeleza na kupima majukumu ya maofisa uhusiano katika maeneo yao ya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,079FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles