24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

GGML waishukuru Serikali kwa kutatua kero, kuikuza sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MAKAMU Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, Simon Shayo ameishukuru Serikali kwa kufanyia kazi baadhi ya mambo yaliyowasilishwa na wadau wa sekta ya madini na kuiwezesha sekta hiyo kuwa kinara kwa ulipaji wa kodi nchini.

Shayo ametoa kauli hiyo leo Oktoba 3, 2022 wakati akizungumza kwa niaba ya wadhamini wakuu katika ufunguzi wa Maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Geita.

Amesema AngloGold Ashanti ambayo ni kampuni mama ya Geita Gold Mining Limited. (GGML), imeendelea kuuthamini mgodi huo na kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha mathalani mwaka 2021 imewekeza kiasi cha Sh bilioni 310.5, mwaka 2022 imewekeza Sh bilioni 388.7 kwa ajili ya upanuzi wa mgodi na shughuli za utafiti na mashapo mapya kwenye migodi mitatu ya uchimbaji wa chini ya ardhi; Nyankanga, Star and Comet na Geita hills. Pia mgodi wa uchimbaji wa wazi Nyamlilima.

“Tunafarijika kampuni (GGML) imeendelea kutambuliwa kama kampuni inayojihimu kuwa walipa kodi wakubwa na kushindana na sekta nyingine ya wazalishaji.

“Tumejitahidi kwenye manunuzi ya ndani, tunakushukuru kwa maelekezo yako (Waziri wa madini- Dotto Biteko) na kutupa walau moyo kwamba tunafanya vizuri kuliko makampuni mengine kwenye eneo la Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR),” amesema.

Amesema GGML itaendelea kujitahidi kwenye maeneo yote kuhakikisha wanatoa mchango kwa Serikali ili kufikia lengo la asilimia 10 la mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa ifikapo 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa GGML katilka nyanja mbalimbali na kuahidi kuwa kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa mlipa kodi bora katika sekta ya madini, itaendelea kuendesha shughuli zake za uchimbaji kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Alitoa wito kwa kampuni nyingine za uchimbaji madini kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuwaletea maendeleo watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles