30.5 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

GGML ilivyong’ara usiku wa madini, yatwaa tuzo mbili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mchango wa Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited (GGML) umeendelea kutambuliwa na wadau mbalimbali wa sekta ya madini kupitia Kongamano la Kimafaifa la Uwekezaji na Madini Tanzania 2023 kutokana na jitihada zake katika uwajibikaji kwa jamii pamoja na kuzingatia afya na usalama mahala pa kazi.

Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang’anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha uhifadhi mazingira, afya na usalama mahala pa kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na Kampuni hiyo kushinda tuzo mbili ambazo ni mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pamoja na uhifadhi wa mazingira, afya na usalama kazini.

Tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya Madini zimeendelea kudhihirisha hadhi ya GGML kuwa mfano wa kuigwa katika masuala hayo ya afya na usalama kazini pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Madini wa Serikali ya Malawi, Monica Chang’anamuno akiongozana na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alikabidhi tuzo hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong pamoja na Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.

Hafla hiyo iliyopewa jina la Usiku wa Madini, ilifanyika tarehe 25 Oktoba 2023 jijini Dar es salaam.

Waziri wa Madini wa Malawi, Monica Chang’anamuno (kushoto) akimkabidhi tuzo ya mshindi wa jumla katika kipengele cha Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), Makamu Rais wa AngloGold Ashati- GGML anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo. Kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde. Hafla hiyo iliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wakifurahia ushindi wa kampuni hiyo iliyonyaku tuzo mbili katika hafla ya usiku wa madini iliyofanyikawiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles