27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Gary Neville atimuliwa Valencia

Gary NevilleVALENCIA, HISPANIA

BEKI wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya England, Gary Neville, amefukuzwa kazi ya kuifundisha klabu ya Valencia ya nchini Hispania, baada ya kuwa kocha kwa miezi minne.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41, ambaye yumo kwenye benchi la ufundi katika timu ya Taifa ya England, alipewa kazi ya kuifundisha klabu hiyo tangu Desemba mwaka jana, lakini juzi uongozi wa klabu uliamua kumfungashia virago vyake.

Klabu hiyo ya Valencia imefanikiwa kushinda michezo mitatu pekee kati ya 16 waliyocheza katika Ligi Kuu ikiwa chini ya kocha huyo, huku akishinda jumla ya michezo 10 kati ya 28 katika mashindano yote.
Neville amesema alitaka sana kukaa katika klabu hiyo, lakini matokeo hayakufikia kiwango chake na viwango vinavyohitajika na klabu hiyo.

“Nilitamani kuendelea kuwa kocha wa klabu ya Valencia, lakini kutokana na matokeo mabaya nadhani uongozi wa klabu haujakubaliana nayo, lakini ninawatakia kila la heri katika safari ya michuano mbalimbali,” alisema Neville.

Hata hivyo, kocha huyo alitaka kujiuzulu mapema Februari mwaka huu baada ya kupokea kichapo cha mabao 7-0 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania, Barcelona, kwenye mchezo wa Kombe la Copa del Rey.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles