25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Eneo la Ikulu lauzwa

Amos Makalla
Amos Makalla

Na PENDO FUNDISHA, MBEYA

MKUU wa Mkoa  wa Mbeya, Amos Makalla, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, kufuatilia eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ikulu ndogo mjini Mbeya, ambalo inasemekana limeuzwa.

Eneo hilo ambalo ukubwa wake haujajulikana, lipo katika eneo la Veta jijini Mbeya na inasemekana limeuzwa kwa wananchi ambao baadhi yao wamejenga nyumba za makazi, huku wengine wakiendelea na ujenzi.

Makalla alitoa agizo hilo jana baada ya kutembelea na kulikagua eneo hilo, huku akishuhudia jinsi baadhi ya watu walivyojenga nyumba zao katika eneo hilo.

“Nimeambiwa eneo hili ni mali ya Serikali lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ikulu, lakini wapo baadhi ya watu wameanza kulitumia kwa kujenga nyumba za makazi.

“Kwa hiyo, nakuagiza wewe mkuu wa wilaya ulifuatilie eneo hili kujua uhalali wake. Nataka ufahamu ukubwa wa eneo, ujiridhishe kama kweli limeuzwa na baada ya hapo, walioliuza wachukuliwe hatua,” aliagiza Makalla.

Wakati Makalla akisema hayo, mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Mbeya ambaye hakutaka kutaja jina lake, aliliambia MTANZANIA kwamba eneo hilo awali lilikuwa likimilikiwa kiasili na wananchi kabla ya Ikulu haijalichukua.

“Hata hivyo, baada ya Serikali kulichukua eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa Ikulu, ilitakiwa kuwalipa wananchi wote waliokuwa wakilimiliki, lakini haikufanya hivyo na badala yake iliwafidia watu wachache.

“Waliolipwa fidia ni wachache kwa hiyo, mtu anaposema eneo la Ikulu limeuzwa mimi napata tabu kumwelewa kwa sababu kuna eneo halikulipwa fidia ingawa Serikali ilikuwa ikilihitaji,” alisema mtoa taarifa huyo.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya (RAS), Mariamu Mtunguja, alipotakiwa na MTANZANIA kutoa ufafanuzi wa eneo hilo, alisema aliomba apewe muda ili afanye uchunguzi wa kina.

“Hapa naona kama kuna mgawanyiko wa taarifa, ninaomba nipewe muda ii nilifuatilie suala hili kwa undani zaidi ili nitakapotoa taarifa iwe ni taarifa sahihi,”alisema Mtunguja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles