23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

EDENVILLE YAANZA UCHIMBAJI MAKAA MAWE RUKWA

Waziri wa Nishati na Madni Prof. Sospeter Muhongo
Waziri wa Nishati na Madni Prof. Sospeter Muhongo

Na Joseph Lino,

Kampuni ya kutoka Uingereza ya Edenville Energy Corporation, imeanza majaribio ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika mradi wake wa kuzalisha umeme wa megawatt 120 mkoani Rukwa.

Mradi huo unahifadhi zaidi ya tani milioni 171 zilizothibitishwa  za makaa ya mawe ambayo yanatosha kutumika kwa kipindi cha miaka 30 cha uhai wa mradi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Edenville Energy, Rufus Short, alisema katika taarifa yake kuwa wamepokea maombi  rasmi kutoka kwa makampuni kadhaa ya kuwasambazia makaa ya mawe ya muda mrefu.

“Majaribio ya usafirishaji wa makaa ya mawe yamekuwa yakisafirishwa kwenda kwa wateja ili wapime ubora, ukubwa wake ambapo wanalipwa kwa ajili ya kupelekewa makaa ya mawe,” alisema Short.

Kwa maelezo ya Edenville, imechukua uamuzi wa kuendelea na mradi huo katika  hatua ya pili ambayo inalenga katika kuanza uzalishaji wa kibiashara na upatikanaji wa vifaa vya uchakataji makaa ya mawe katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kwa upande mwingine, kampuni itaweka mitambo ya kusafisha makaa ya mawe katika eneo hilo na pia makaa ya mawe mengine yatakuwa yanasambazwa bila kusafishwa.

Hata hivyo, makaa ya mawe mengi yatapitia katika mchakato maalumu wa kusafishwa ili kupata bidhaa bora mbalimbali kwa wateja tofauti ili kuleta matokeo yenye tija kwa Edenville.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles