25.5 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Dumisheni Amani ili duniania iwe mahala salama pa kuishi-Lee Man-hee

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jumla ya Wanafunzi 108,084 wa masomo ya biblia wamehitimu mafunzo yao katika kituo cha Umisheni ya Kikristo cha Sayuni kilichoko nchini Korea Kusini.

Katika mahafali hayo ya 114 yaliyofanyika katika uwanja wa Daegu kwa mwaka huu ndiyo yamekuwa na wahitimu wengi zaidi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Matharani mwaka 2019 wahitimu ya fani hiyo chuoni hapo walikuwa ni 103,764 huku mwaka 2022 wakiwa ni 106,186.

Miongoni mwa wahitimu hao ni Wachungaji 6,724 wa zamani na wa sasa kiwango ambacho ni mara 10 zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.

Akizungumza katika mahafali hayo Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji la Yesu,Lee Man-hee alisisitiza watu kuifanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi.

“Mungu atakuwa akiangalia mkutano wetu. Tuifanye dunia kuwa mahala pazuri zaidi kulingana na mapenzi ya Mungu,” alisema Lee.

Katika hotuba yake ya pongezi, Mkurugenzi Mkuu Tan Young-jin wa Kituo cha umisheni ya Kikristo cha Sayuni alisema, “Wahitimu walisikia moja kwa moja neno kubwa zaidi lililofunuliwa la miaka 6,000 na kuthibitisha kile Mungu ameahidi leo. Kwa hiyo, naamini kwamba umetambua wazi wewe ni nani kama ilivyosemwa katika Biblia.

“Sasa hebu tuwe mstari wa mbele katika kufufua mataifa yote na kufikia amani ya ulimwengu,” alihimiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles