28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Samia alivyoibuka kidedea CCM

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa Mwenyekiti CCM kwa miaka mitano tangu 2022 hadi 2027 kwa kura 1,914 kati ya 1,915.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, ni kura moja tu ya hapana na hakuna kura iliyoharibika.

Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa Juu wa CCM jioni ya Desemba 7, 2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Muda Dk. Mohammed Ali Shein alisema kwa ushindi huo wa kura anamtangaza Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Aidha, Dk. Shein alimtangaza mrithi wake Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar baada ya kupata kura 1,912 kati ya 1,915 zilizopigwa.

Dk. Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anachukua nafasi hiyo baada ya Dk. Shein kumaliza muda wake. Dk. Mwinyi alipata kura za hapana tatu.

Katika uchaguzi huo pia alimtangaza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Komrade Abdurahman Kinana kwa kupata kura 1,913 kati ya 1,915. Kinana amepata kura za hapana mbili.

Pia, Dk. Shein aliwatangaza washindi wa nafasi 40 za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambao kati ya 20 wanatoka Zanzibar wakiwemo wanaume 14 na wanawake sita na vilevile wajumbe 20 kutoka Bara wakiwemo wanaume 14 na wanawake sita.

Katika uchaguzi wa wajumbe wa NEC walikuwa katika mnyukano mkali lakini baadhi ya majina ya mawaziri, wabunge na watendaji serikalini waliokuwa wakitajwa sana wameshindwa kupenya na huku sura mpya ziking’ara ambazo Ilikuwa zikipewa nafasi ndogo katika pande zote mbili za Muungano Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kiti, Mwenyekiti wa Chama Dk. Samia aliwapongeza wajumbe kwa kuchagua yeye na viongozi wenzake katika chama.

Pia alimpongeza mwenyekiti wa muda Dk. Shein kwa kuendesha uchaguzi vizuri pamoja na kamati ya uchaguzi pamoja na wasaidizi wao kwani wakati wanapanga ratiba walijua wangekesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles