24.3 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwigulu akaribisha uwekezaji sekta ya nishati

Na Scola Malinga, WFM, Dar es Salaam        

WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba ameikaribisha taasisi ya kifedha ya Uingereza inayojihusisha na uwekezaji (British International Investment) kufanya uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo ya Nishati.

Dk. Nchemba, ametoa wito huo alipokutana na kufanya majadiliano na ujumbe wa British International Investment, katika Ofisi ya Hazina, jijini Dar es Salaam ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya ushirikiano wa maendeleo.

Dk. Nchemba ametaja maeneo muhimu ya uwekezaji katika sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na usambazaji wa umeme, kuwekeza katika mafuta na gesi kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye akiba kubwa ya hydrocarbon yenye gesi na mafuta.

Amesema kuwa maendeleo ya miundombinu hiyo ni kipaumbele kikubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania na inatarajia kuwa na matokeo makubwa na ya haraka katika kuongeza ajira na kukuza kipato.

Amesema maeneo mengine muhimu ambayo Serikali imeweka jitihada ni pamoja na Ushirikiano wa Umma na Binafsi (PPPs) katika sekta za uzalishaji ambazo zina jukumu muhimu katika kuendesha maendeleo endelevu nchini.

Aidha, Dk. Nchemba ameziagiza timu za wataalam kuhakikisha zinafanya majadiliano ya kina kuhusiana na uwekezaji ambao taasisi hiyo imeonesha nia ya kufanya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya British International Investment, Simon Cheung, amesema taasisi yake ipo tayari kufanya majadiliano na Serikali ya Tanzania na kuipa kipaumbele kwenye kusaidia kuwekeza katika maeneo mbalimbali.

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Taasisi ya kifedha ya uwekezaji ya Uingereza, Simon Cheung (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Taasisi hiyo,  Ope Onibokun (wa pili kulia), Mkuu wa masuala ya Uwekezaji kwenye Miundombinu, Tabish Shariff (kushoto) na kulia ni Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha, Japhet Justine.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dar es Salaam)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles