22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Chana atoa kwa wadau wa Utalii kuchangamkia fursa kupitia S!TE

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana ametoa wito kwa wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili International Tourism Expo (S!TE).

Akizungumza Dar es Salaam leo Julai 20, 2022 Dk. Chana amesema onyesho hilo litafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 21 hadi 23, Mwaka huu.

Amesema onesho hilo kubwa la utalii ambalo ni la Sita litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam Tanzania.

Alisema fursa zitakazotangazwa katika onesho hilo Ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho hilo.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali yatajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE” ameongeza Chana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles