24.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Dk. Bashiru: Serikali hii imedhamiria kuondoa rushwa

Na Mwandishi Wetu Fujian, China

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally, amesema Serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, imejizatiti kuondoa rushwa.

Dk. Bashiru alisema hayo jana katika Kaunti ya Shaxian jimbo la Fujian nchini China alipokutana na gavana wa kaunti hiyo ambaye alieleza walivyofanikiwa kuondoa umaskini kwa wananchi wao na uboreshaji wa makazi na miundombinu.

Katika mazungumzo hayo Dk. Bashiru alisema licha ya vita ya rushwa kuwa kubwa na ngumu, lakini hawatachoka kwani mafanikio ya vita hiyo yameanza kuonekana.

Kiongozi huyo alisema kupitia ziara ya makada wa CCM nchini China wamegundua uzalendo, nidhamu na uwajibikaji ndivyo vilivyoifikisha China kuwa mbali katika maendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Kheri James amesema kupitia ziara hiyo ya mafunzo atahakikisha vijana nchini wanawekewa mazingira rafiki ya kuhakikisha wanatumia vipaji vyao kubuni miradi ya kimaendeleo ili kulisaidia Taifa.

Dk. Bashiru na ujumbe wake yupo nchini China kwa ziara ya siku kumi kwa mwaliko wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho ni chama rafiki na CCM ili kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles