23.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

DC Jokate akabidhi nyumba 8 kwa watoto wanaoishi mazingira hatarishi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Jokate Mwegelo amekabidhi nyumba nane kwa Watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 50.

Nyumba hizo zimejengwa kwa ufadhili wa pamoja kati ya Kanisa la Anglican Msambiazi pamoja na KKKT Emao Old Korogwe ikiwa na lengo la kuwanufaisha watoto hao kutoka katika wimbi la umasikini.

DC Jokate amesema: “Rai yangu kwa hawa waliopatiwa nyumba hizi nane wasije wakatumia nyumba hizi kwa kuziuza au kupangisha kwanza ifahamike nyumba hizi ni za hawa Watoto kwahiyo Wazazi wanakaa kama Walezi tu wa kuwasaidia kuzishika lakini kwenye zile hati za makabidhiano majina yaliopo ni ya Watoto husika,“ amesema Jokate.

Awali, akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo Mratibu wa Kituo cha Watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi Anglican Msimbazi Mery Msendekwa amesema kuwa Kanisa la KKKT EMAO limejenga nyumba nne na Anglican Msambiazi limejenga nyumba nne huku zote zikiwa na thamani ya Sh milioni 50.4

Mchungaji na Mlezi wa kituo cha Anglican Msimbazi Canon, Jackson Matunga amesema lengo ni kuwawezesha Watoto hao kuishi mazingira mazuri na nyumba hizo ni mali za Watoto na endapo Mtoto atanyanyaswa kupitia nyumba hizo Kanisa litasimama na kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles