23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

DC Ileje akanusha uvumi wa shule kutelekezwa

Na Denisi Sikonde, Ileje

Serikali imekanusha uvumi wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba imeitelekeza shule ya msingi Kaguru iliyoko wilayani Ileje mkoani Songwe.

Hayo yamebainishwa Aprili 11, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya baada ya kutembelea na kukagua hatua za ukarabati wa shule hiyo ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali.

Gidarya amesema kuwa serikali imeendelea kuboresha miundombunu ya shule hiyo iliyojengwa na wananchi wa kitongoji cha Chafwonywa kilichopo Kijiji cha Itumba kata ya Itumba wilayani humo na kwamba haijaitelekeza kama inavyozushwa.

“Nimetembelea shule hii kwa ajili ya kujionea ukarabati wa miundombinu mbalimbali kwani kumekuwa na uvumi kwamba serikali imetelekeza shule hii jambo ambalo siyo kweli hata kidogo, kwani imeendelea kuitengea fedha ya kukarabati miundombinu mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi.

“Kuhusu maelezo ya vyoo kama ambavyo imekuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamiii, tayari vimejengwa ikiwamo miundombinu ya sinki kwa nguvu ya serikali kwa kwa kushirikiana na mbunge pamoja na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Ileje,” amesema Gidarya.

Akizungumzia upatikanaji wa maji shuleni hapo, Gidarya amesema tayari wamezungumza na wakandarasi wa maji kwa ajili ya kuhakikisha ustawi wa shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kuendelea kufanya ujenzi wa madarasa mengine kwania tayari wamepata zaidi ya Sh milioni 40 kutoka serikalini.

Upande wake Afisa Elimu Msingi wilayani Ileje, Fikiri Mguye amesema tayari serikali ipo kwenye mpango wa kuhakikisha inaboresha mazingira ya shule hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

“Kwa kushirikiana na wananchi serikali imepata mradi wa Boost kwenye Program ya Lanes II na kufanikiwa kupata fedha milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya shule hii ili kuboreshwa miundombunu ya shule hii iliyojengwa na wananchi mwaka 1995,” amesema Mguye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles