22.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 5, 2022

DC Ileje aitaka jamii kutowaficha watu wenye ulemavu siku ya Sensa

Na Denis Sinkonde, Songwe

Kuelekea Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23, mwaka huu jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu ili kuiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupata taarifa sahihi za kundi hilo zitakazotumika kutekelezea mahitaji yao kwa ufanisi.

Wananchi wakimpokea Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna GIdarya (aliyevaa miwani) ambaye pia aliambatana na Diwani wa Sanfe, Kaptoni Ngabo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Agosti 18, 2022 katika Kijiji cha Lusalala kata ya Sange wilayani humo, ambapo moja ya ajenda zake ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa bila kulisahau kundi la watu wenye mahitaji maalumu ifikapo Agosti 23.

Gidarya amesema kutokana na kutokuwepo kwa takwimu sahihi za watu wenye ulemavu imekuwa sababu kubwa kwa serikali kushidwa kutimiza mahitaji ya kundi hilo, hivyo jamii inapaswa kushirikiana na viongozi wa maeneo yao kuwaandikisha siku ya zoezi la sensa.

Amefafanua kuwa kitendo cha jamii kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi wanaikosesha serikali fursa ya kupata takwimu sahihi ambazo zingetumika kuwasaidia katika kero mbalimbali zinazowakabili.

“Kwa mfano Ileje ina watoto wengi wenye ulemavu, hivyo basi jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa kuwakumbusha kuwahesabu walemavu kwenye kaya zitakazokuwa na nia ovu ya kuwanyima haki ya kuhesabiwa,” amesemai Gidarya.

Rehema Kayuni mkazi wa Kijiji hicho ambapo amesemakuwa elimu inayotolewa na viongozi juu ya sensa hususan utambuzi wa watoto wenye ulemavu iwe jukumu la jamii nzima kwani baadhi yao hufichwa kwa kigezo cha kutotambuliwa wakijua ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Jobu Kabuje mkazi wa Kijiji hicho amesema jamii hainabudi kupewa elimu juu ya kushiriki zoezi la sensa kwa kuhamasisha kundi la watu wenye mahitaji maalumu bila kuwaficha kwani nao wanapaswa kutambuliwa ili mahitaji yYao yaweze kubainishwa kitaifa.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Abeli Mwakachela ambaye ni Mwenyekiti wa wa watu wenye ulemavu Mmkoa wa Songwe amesema kundi hilo ni muhimu kuendelea kupewa elimu ili waweze kuwa na uelewa wa kusaidia kurahisisha zoezi.

Mwakachela ameongeza kuwa japokuwa siku zimebaki chache lakini elimu kwa mwananchi ni muhimu juu ya dodoso la faragha ikiwepo kwenye kundi la watu walemavu, kwani linawachanganya watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,751FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles