28.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

DC Hai avunja mabaraza ya ardhi ya kata

Omary Mlekwa, Hai

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ameagiza kuvunjwa kwa mabaraza ya ardhi ya kata tatu ndani ya saa 24, kutokana na kulalamikiwa na wananchi kuhujumu haki za wananchi katika kumiliki ardhi.

Mabaraza hayo ni Machame Magharibi, Bomang’ombe na Bondeni pamoja kamati za ardhi vijiji vya Mkalama, Kawaya na Rundugai.

Amri hiyo ameitoa leo Alhamisi Machi 14, katika mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, migogoro na malalamiko ya ardhi ya wananchi kata 17 za wilaya hiyo ambapo pia amesema mabaraza hayo yamekuwa chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi.

“Hadi kufikia jana nilikuwa nimepokea malalamiko, migogoro na kero 266 ambazo ni kusogeza mipaka, urasimishaji makazi, fidia ya ardhi na zoezi la uwekaji alama za mipaka.

“Nakuagiza mwanasheria wa halmashauri (Henglibert Boniface) kwa kushauriana na mkurugenzi wako mtendaji ikifika kesho mniletee taarifa kuwa mmeshavunja mabaraza hayo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles