30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

DC awataka vijana kumuunga mkono Rais magufuli

Mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi amesema vijana nchini wanapaswa kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli kwa jinsi alivyowaamini kwenye nafasi mbalimbali za uongozi

Ndejembi amesema kwa miaka mingi kulikuwa na dhana ya vijana kuonekana hawana uwezo wa kuongoza lakini Rais Magufuli ameteua vijana wengi kwenye uongozi kuliko awamu nyingine zote na kwamba anapaswa kuungwa mkono na vijana na siyo kulalamika pembeni.

“Leo hii chini ya Rais Magufuli Tanzania imepiga hatua kwenye sekta ya usafirishaji, tunajenga reli ya kisasa kiwango cha Kimataifa (SGR), usafiri wa anga ulikua umekufa lakini tunavyozungumza ndege zinapishana angani kutua viwanja vya Afrika Kusini na India hivyo ni lazima tumuunge mkono Jemedari wetu huyu,” amesema Ndejembi.

“Ninapoona mtu analalamika ninashangaa sana, ndani ya kipindi cha miaka minne yamefanyika mambo makubwa ambayo kwa muda mrefu yalishindikana, uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye nishati na umeme ambapo mradi mkubwa wa Stiglers unajengwa, umeme umefika hadi kijijini na kule kukatika katika kwa umeme migao ya mara kwa mara imekwama.

“Sisi vijana tulioamiwa na Rais tuna jukumu zito la kumsaidia kazi, kutekeleza yale yote ambayo amekua akihitaji kuona Watanzania wanyonge wananufaika na nchi yao lakini pia ndani ya chama chetu cha CCM tuko imara chini ya Mwenyekiti wetu Dk. John Magufuli, “amesema Ndejembi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles