22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

CUNEYT CAKIR KUWAHUKUMU CROATIA, ENGLAND

MOSCOW, URUSI


MWAMUZI kutoka nchini Uturuki, Cuneyt Cakir, amepewa nafasi ya kuchezesha mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia kati ya England dhidi ya Croatia, kwenye Uwanja wa Luzhniki.

Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 41, ameweza kuchezesha makundi mawili kwenye michuano hiyo nchini Urusi, alisimama katikati katika mchezo wa Iran ikishinda bao 1-0 dhidi ya Morocco, Argentina ikiingia hatua ya 16 bora kwa kuwafunga Nigeria mabao 2-1.

Katika michezo hiyo yote aliweza kutoa jumla ya kadi tisa za njano na alitupiwa lawama katika mchezo huo dhidi ya Nigeria kwamba hakutenda haki kwa timu hiyo kutoka Bara la Afrika.

Cakir amekuwa akifanya kazi ya uamuzi tangu akiwa na umri wa miaka 17 na amekuwa akiaminiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Mwamuzi huyo alichezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015, huku Barcelona ikitwaa ubingwa dhidi ya Juventus, pia alichezesha nusu fainali ya michuano hiyo katika hatua ya nusu fainali kati ya Real Madrid dhidi ya Bayern Munich mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles