31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

CRDB yaja na kampeni ya matumizi ya kadi

NA LOVENESS BERNARD -DAR ES SALAAM

BENKI ya CRDB kwa kutambua mchango wa wateja wake, imeamua kuanzisha kampeni maalumu ya matumizi ya kadi kufanya malipo ijulikanayo kama “Chanja, Lipa, Sepa’’.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jana Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Huduma Mbadala wa benki hiyo, Farid Seif.

Alisema kampeni hiyo itawafanya wateja kupata punguzo kwa baadhi ya maduka yaliyochaguliwa.

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha wateja wote wa Benki ya CRDB kutumia Tembo Card Visa na SimBanking Visa kufanya malipo yao ya manunuzi. Lengo letu ni kuona Watanzania wanaondokana na matumizi ya pesa taslimu na kutumia mifumo hii ya kidijitali ambayo ni rahisi, salama na nafuu kufanya malipo.

 “CRDB ikiwa kama benki inayoongoza kwa ubunifu wa huduma na bidhaa katika soko, mwaka 2002 tulizindua huduma ya TemboCard, ikiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania na wateja wetu kuweza kupata huduma za kibenki kwa uharaka, usalama na unafuu,” alisema Seif.

Alisema pamoja na mafanikio hayo makubwa, wateja wengi bado hawana utamaduni wa kutumia TemboCard zao kufanya malipo, kitu ambacho kinawasababisha kukosa baadhi ya huduma.

“Hivyo basi, leo hii (jana) Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Visa International tunazindua kampeni maalumu ya kuwahamasisha wateja na Watanzania kwa ujumla kutumia kadi zao kufanya malipo, kampeni ambayo tumeipa jina la “Chanja, Lipa, Sepa,” alisema Seif.

Alisema kuwa ili kushiriki katika kampeni hii mteja anatakiwa kutumia kadi yake ya TemboCard Visa au huduma ya Sim Banking Visa kufanya malipo ya manunuzi katika supermarkets, maduka ya rejareja, migahawa, baa, hoteli na sehemu mbalimbali zinazopokea malipo kwa njia ya kadi au QR Code ikiwamo mtandaoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles