24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Chenge akabidhi Kompyuta tano Shule ya Sekondari Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mtemi Andrew Chenge amekabidhi Kompyuta tano na Mashine ya kuchapisha kwa shule ya sekondari Simiyu iliyoko mjini Bariadi.

Kompyuta hizo zimetolewa na mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa ajili ya kuunga mkono utekelezaji wa mkakati wa kufundisha wanafunzi kwa njia ya mtandao.

Akikabidhi msaada huo mke wa mbunge huyo, Tina Chenge, mbele ya Mkuu wa Mkoa, Antony Mtaka amesema kuwa Kompyuta hizo zitasaidia kuinua kiwango cha elimu katika wilaya hiyo.

Amesema kuwa mbunge huyo aliamua kutoa vifaa hivyo kwa shule hiyo ili kiwe kituo cha taaluma bora katika Mkoa wa Simiyu kwani kitasaidia kuboresha hali ya elimu mkoani humo pamoja na shule yenyewe.

Akipokea vifaa hivyo Mtaka, amemshukuru mbunge kwa msaada huo, n na kusema msaada huo utasaidia utekelezaji wa mpango mkakati mpya wa kufundisha watoto kwa anjia ya mtandao.

” Katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na janga la corona, tumezindua mkakati huu ili wanafunzi wafundishwe kwa njia ya mtadao na msaada huu umekuja wakati muafaka,” amesema Mtaka.

Naye Mkuu wa shule hiyo, Paul Susu amemshukuru Chenge kwa msaa huo, ambao utasaidia kuendeleza jitihada walizoanza za kufundisha kwa njia ya mtandao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,249FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles