Chanjo husaidia ubora kinga ya mwili

0
689

AMINA OMARI-TANGA

IMEBAINIKA kuwa mwili wa binadamu unavyopata chanjo kwa wingi zinasaidia  kuongeza  ubora wa kinga ya mwili.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa chanjo Mkoa wa Tanga, Seif Shaibu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo namna ya kuripoti habari kuhusu chanjo.

Alisema kuwa mwili wa binadamu unakabiliana na changamoto nyingi za madhara hivyo chanjo zinasaidia kuimarisha kinga ya mwili na kuweza kupambana na maradhi hayo.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa chanjo ni muhimu kwa kuwashauri wazazi na walezi wenye watoto chini ya miaka mitano kuhakikisha wanapata chanjo zote ili mwili uweze kujijenga .

Shaibu alisema kuwa kinga ni bora kuliko tiba kwani kuna baadhi ya maradhi yanaposhambulia mwili wa binadamu haya tiba lakini Kama umepata chanjo unaweza kuyadhibiti.

“Niwaombe wananchi mkisikia kampeni za chanjo nendeni haraka mkapate kwani zinasaidia kuimarisha Kinga za mwili dhidi ya kushambuliwa namagonjwa,” alisema

Hivyo aliwashauri wazazi wenye watoto chini ya miaka mitano kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya ilikuweza kupatiwa chanjo ya surua, polio na rubela .

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga, Hassan Hashim alisema kuwa elimu hiyo ya chanjo ni vema ikawa inatokewa mara kwa mara ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa chanjo.

“Bado jamii haijaweza kupata uwelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa chanjo kwani kuna watoto wengi ambao wanashindwa kukamilishiwa chanjo kwa wakati wake,” alisema Hashim.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here