28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea adai kuzuiwa kufanya shughuli za jimbo

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MBUNGE  wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema),  amesema anatarajia kumwandika barua Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na Spika wa Bunge Job Ndugai kutokana na kuzuiliwa kufanya shughuli zake za kijimbo  katika jimbo lake kwa kile alichoeleza hafahamu sababu.

Alizitaja baadhi ya shughuli alizotaka kufanya jimboni hhumokuwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi wake kuhusu ujenzi wa Daraja katika Mto Gide lililopo katikati ya Makoka na Kimara Baruti ambapo mvua zilizonyesha juzi zilileta maafa na mtoto ajulikanae Rashid Makaye alitumbukia katika daraja hilo namwili wake kushindwa kupatikania mpaka leo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa ugawaji wa mihuri ya chama katika jimbo lake itakayotumika kuthibitisha mgombea, alisema atamwandikia barua Msajili wa Vyama vua Siasa na Spika wa Bunge  na kuambatanishia  barua zote za polisi na video za juzi alizozuiliwa asifike katika mkutano wake na wananchi.

Alisema endapo madai hayo hayatasikilizwa atakiahirikiaha chama chake ili kiweze  kuandika malalamiko rasmi kwenye Jumuiya ya Kimataifa.

Alisema wamechoka kuzuiwa kufanya mikutano na wananchi huku wanachama wa CCM wakiendelea na shughuli mbalimbali ikiwemo hata ile ya CCM ya Kijani inayoendelea kila jimbo.

Alisema kuzuiwa kwa mikutano hiyo kumemdhoofisha juhudi zake katika kukutana na wananchi katika kusikiliza kero zao na kuwatumikia wananchi wake.

“Naamini kuwa kuzuiliwa kwangu kufanya mikutano jimboni ni kwa sababu yeye ni miongoni mwa wabunge wanaofanya kazi kubwa ndani ya kipindi kifupi ya kuwatumikia wananchi na kuwapelekea maendeleao,”alisema Kubenea.

Alieleza shughuli mbalimbali alizofanya katika fedha za mfuko wa jimbo kuwa ni pamoja na kununua milioni nane kwa ajili ya kujenga kisima katika Shule ya msingi Mabibo na kutoa milioni 12 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima katika Soko la Gamesi lililopo Mabibo ili wafanyabiashara wa soko hilo wapate maji.

Wakati huo huo Kubenea aligawa mihuri 46 ya mitaa yote ya jimbo lake ambayo itatumika katika ujenzi wa Chama na kwenye Uchaguzi wa Serikali ya mitaa ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles