30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

CCM KUJADILI AGIZO LA JPM HATIMA YA MADIWANI

 

Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA


VIKAO vya kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu yaChama cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Arusha vinatarajiwa kuanza leo.

Pamoja na mambo mengine watajadili majina ya wagombea wa udiwani katika uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Pamoja na hali hiyo kikao hicho o pia kitajadili agizo la Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. John Magufuli kuhusu madiwani waliojiuzulu nafasi zao na kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM  ambao wengi wao wameshindwa katika kura za maoni.

Akiwa katika ziara mkoani hapa, Rais Magufuli  aliagiza madiwani waliojiuzulu na kujiunga na CCM wapewe fursa ya kuwania tena nafasi hizo kupitia CCM.

Akizungumza na MTANZANIA   mjini hapa jana, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,  Shaban Mdoe alisema baada ya kufanyika  kura za maoni za ndani kwa ngazi ya kata, CCM inakutana na kuanza mchujo wa majina ya wagombea wa nafasi hizo.

Alisema kwa sasa hakuna mwanachama anayeweza kujitangaza hadharani kuwa ndiye atapeperusha bendera ya CCM pamoja na kuwa baadhi yao walitangazwa kuwa wamepata kura nyingi kuliko wengine.

“Tunatarajia kuwa na vikao vya kamati ya siasa ya mkoa na kile cha halmashauri ya mkoa ndiyo utaratibu wetu kuyapitia majina yote bila kujali kiasi cha kura.

“Lengo ni kujiridhisha iwapo walioshinda walishinda kwa halali au walitumia rushwa.

“Wewe ni shahidi wa jinsi CCM ya sasa inavyopiga vita rushwa kwa vitendo, viongozi wa ngazi zote wanavyofanya kazi ya kuwatumikia umma.

“Tunazo kanuni zetu tutazitumia, tunayo katiba yetu tutaitumia lengo ni kuhakikisha mwanachama anayepita haendi kutupa kazi kubwa ya kumnadi mbele ya wapiga kura,” alisema Mdoe.

Madiwani hao ambao awali walishinda nafasi hiyo kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita na sasa wameshindwa katika kura ya maoni ndani ya CCM ni Anderson Sikawa (Leguruki), Grayson Issangya (Maroroni) Emanuel Mollel (Makiba) na Japhet Jackson (Embureni).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles