CCM Dodoma wajiandaa kunufaika

Salum KalliNa SARAH MOSES, DODOMA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Dodoma Mjini, kimejipanga kutumia fursa ya Serikali kuhamishia makao makuu mkoani hapa kwa mali zake kutumiwa na watakaokuja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kaimu Katibu wa Chama hicho, Salum Kalli, alisema watatumia fursa hiyo kupitia viwanja na miradi mbalimbali waliyonayo.

“Kwanza kabisa, tunampongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.

“Tupo tayari kutoa ushirikiano utakapohitajika kwani tunaamini tutanufaika kupitia ujio wa wageni wengi mkoani hapa,” alisema Kalli.

Aliitaja baadhi ya miradi waliyonayo kuwa ni pamoja na Uwanja wa Mpira wa Jamhuri na maeneo mengine ya biashara.

Pamoja na hayo, aliwaasa wana CCM kuitumia fursa hiyo kwa kufungua biashara mbalimbali zitakazowasaidia kuongeza kipato chao ili kuepuka maisha ya kuombaomba.

Pia, aliwashauri viongozi washirikiane kikamilifu ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kuzitatua kero mbalimbali za wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here