24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

CAG kuitikia wito wa Spika Ndugai

Na Mwandishi wetu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad, amesema ataitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Januari 21, mwaka huu, kama alivyotakiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Aidha, amesema majibu yake katika mahojiano yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kulidhalilisha bunge.

Hatua hyo ya CAG imekuja siku chache baada ya Spika kumtaka kuripoti katika Kamati hiyo ya Bunge, Januari 21 mwaka huu kutokana na kauli yake ya kusema kuwa bunge ni dhaifu wakati akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa nchini Marekani, hivi karibuni.

“Maneno kama udhaifu na mapungufu ni lugha ya kawaida sana kwa wakaguzi katika kutoa maoni ya utendaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali,” amesema Profesa Assad akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Januari 17.

Amesema ni wazi kuwa watu wengine wanaweza kuchukua tafsiri tofauti ya maneno kama hayo ambayo yamesababisha malumbano makali na marefu katika nyanja zote za mawasiliano kuhusu rai na nafasi na maamuzi mbalimbali yaliyochukuliwa na viongozi mbalimbali na wanadiasa.

“Januari 15, nilipokea wito wa kisheria ulionitaka kutokea mbele ya kamati ya bunge tarehe 21 Januari mwaka huu, kwa mantiki ya kudumisha mahusiano mazuri kati ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali na Bunge, ninayo nia ya kuitikia wito huo hapo tarehe 21,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles