28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

BoT yafafanua sababu za ongezeko la Riba

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imefafanua sababu ya ongezeko la Riba ya Benki Kuu ya asilimia sita kuwa inalenga kudhibiti mfumuko wa bei siku za usoni.

Akizungumza leo Aprili 8,2024 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BoT, Dk. Suleiman Missango amesema mwenendo wa uchumi wa dunia ulikuwa unaashiria uwepo wa mfumuko wa bei hivyo ikaona iongeze riba kutoka asilimia 5.5 hadi asilimia sita katika robo ya pili kuanzia Aprili mwaka huu.

Amesema kupanda kwa riba hiyo kumezingatia ukuaji wa uchumi kwa maana ya uwepo wa fedha za kutosha katika mzunguko kulingana na malengo yaliyowekwa.

“Wengi walijua tunakwenda kuweka ukomo wa riba sio kweli, kwa kupandisha riba hiyo maana yake tunapunguza ukwasi katika mzunguko na hivyo kudhibiti mfumuko wa bei kwa siku zijazo.

“Kupanda kwa riba hiyo kumezingatia ukuaji wa uchumi, maamuzi mengine yatachukuliwa Julai mwanzoni na riba hii ni ya robo ya kwanza ya Aprili, mwaka huu na inaweza kupungua au kuongezeka kwa kadri ya uchambuzi utakavyokuwa,” amesema Dk. Missango.

Amesema Benki Kuu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na mabenki ili kudhibiti ujazi wa fedha katika mabenki nakwenye mzunguko.

“Tangu Benki Kuu ianzishe mfumo wa riba ya Benki Kuu mwaka huu badala ya mfumo wa zamani wa ujazi wa fedha hali imeendelea kuwa tulivu na mapokeo yamekuwa mazuri kwa wadau,” amesema.

Ameeleza kuwa hali hiyo imetokana na juhudu kubwa ya kutoa elimu kwa wadau katika sekta na imeahidi kuendelea kutoa elimu kwa wanananchi kuweza kufanya uamuzi sahihi katika shughuli za kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles