24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Biteko awataka wananchi kulinda rasilimali za madini

HADIJA OMARY, MTWARA

Waziri wa Madini Dotto Biteko, amewataka wananchi kulinda rasilimali za madini nchini ikiwa ni pamoja na kutumia utajiri wa madini uliopo kubadilisha maisha yao.

Biteko ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pachani Wilaya Nanyumbu Mkoani Mtwara, juu ya kusitishwa kwa shughuli ya uchimbaji wa madini ya chuma iliyokuwa inaendea  Kijiji hipo.

Amesema kuwa kwa miaka mingi utajiri wa madini yaliyopo nchini yalikuwa yakiwanufaisha wageni huku wenyeji wakiwa bado wanabaki masikini licha ya rasilimali hizo kuwepo kwenye maeneo yao.

“Tanzania ni moja kati ya nchi tajiri kwa madini duniani, hata kwa Afrika nzima sisi ni wanne kwa madini ya dhaabu, wapili kwa madini ya vito, tunayo madini mengine mengi ambayo hayapatikani mahali pengine isipokuwa Tanzania nayo ni Tanzanite” amesema.

“Haiwezekani tuna utajiri huo alafu watu wetu bado ni masikini ndio maana Rais wetu mnamsikia kila wakati anasema Tanzania sio masikini, unaweza ukasema kuwa wewe ni masikini iwapo hautumii kisawasawa uwezo wako wa kufikiri,” amesema.

Aidha amesema kuwa  lengo la serikali la kubadilisha sheria ya madini ni kutaka kuona rasilimali hiyo inawanufaisha Watanzania ili madini  yanayopatikana nchini yawe chachu ya kubadilisha maisha ya wananchi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles