23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Bilioni 9 zalipwa Ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji

Na Abubakari Akida,Dodoma

Jumla ya Sh bilioni 9.1 zimelipwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMA JKT ikiwa ni sehemu ya malipo ya gharama ya Ujenzi wa Mradi wa Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma ambao kukamilika kwake utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 20.

Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji,Issa Mohamed akiongozana na  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo(katikati) na  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk.Anna Makakala  (wakwanza kushoto) wakati wa ziara ya Naibu Waziri   kukagua ujenzi huo ambao mpaka kukamilika kwake itagharimu kiasi cha Bilioni 20 ikiwa ni fedha za ndani.Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dodoma..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Juni 25, 2021 na Mhandisi wa Mradi huo, Issa Mohammed akisoma taarifa ya mradi huo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu.

“Lengo letu ni kumaliza mradi huu katikati ya mwezi Oktoba, pamoja na kuzingatia muda bado tunachukua tahadhari kubwa kuhakikisha ubora na uimara unaotegemewa kufikiwa kuanzia kwenye msingi hadi kukamilisha mradi mzima huku tayari tukiwa tumeshalipwa kiasi cha fedha Bilioni 9.1/=  hii ikijumuisha malipo ya awali kwa ajili ya watoa huduma  ambayo thamani yake ni Bilioni 1.3,” amesema Mhandisi Issa.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo alisema miradi hii iliyoachwa na Hayati John Magufuli ni muhimu imalizwe ili kiasi hicho cha fedha za Watanzania kitumike ipasavyo.

“Miradi hii imetumia fedha nyingi tena fedha zetu za ndani,ifike wakati miradi hii ikamilke  maana hakuna fedha iliyotoka nje kwa maana msaada kwahiyo kazi iendelee ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, nawaomba wafanyakazi wafanye kazi usiku na mchana ili jengo hili lianze kutumika kama lilivyokusudiwa,” amesema Naibu Waziri Khamis.

Mradi huo ulianza rasmi tarehe 28 Mei mwaka 2019 ukijumuisha ujenzi wa jengo la Ofisi lenye urefu wa ghorofa nane na sakafu ya chini, uwekaji wa mifumo ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na kusawazisha ardhi ya nje ya jengo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles