23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bawacha yawakana akina Mdee, sasa kutinga mahakamani

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bawacha) limesema litaenda Mahakamani kupinga ubunge wa Wabunge 19 wa Chama hicho ambapo limeendelea kusisitiza haliwatambui na walishavuliwa uanachama.

Pia, limeweka ushahidi wa barua ambayo walimtumia Spika wa Bunge, Job Ndugai ya Wabunge hao 19 kuvuliwa uanachama.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson jana bungeni kusema kwamba wanawatambua Wabunge hao 19 ni wa Chadema na wala hawajawahi kupokea taarifa ya kuvuliwa uanachama Wabunge hao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jumamosi April 24, Mwekahazina wa (Bawacha), Catherine Ruge amesema wao kama Baraza wataendelea kupaza sauti kuhakikisha katiba inalindwa kwani imekuwa ikisiginwa juu ya Wabunge hao.

Amesema wataenda Mahakamani kulinda na kutetea katiba kuhusiana na uhalali wa Wabunge hao.

“Sisi Baraza tutaendelea kupaza sauti juu ya uvunjwaji wa Katiba, kwahiyo Baraza la Wanawake tutaenda mahakamani kuhakikisha Katiba yetu inalindwa,”amesema Catherine.

Amesema Kamati kuu ya Chama hicho haijawahi kuteua majina hayo 19 na wale waliopo Bungeni walijiteua wenyewe.

Alipoulizwa Je watateua wengine,Ruge amesema: “Siwezi kusema mpaka vikao halali vikae,”

Amesema wao wanaushahidi barua ya kuwavua uanachama Wabunge hao kwani walimpelekea Spika na mtumishi wa Bunge alisaini katika Dispatch
.
“Hili ni jambo la dharau, hatujui Kuna siri gani kati ya Spika na wale Wabunge ni kitu kibaya sana,” amesema.

Amesema wanamuomba Spika ajitokeza na akiri hadharani kwamba amepokea taarifa rasmi na aseme wamepoteza sifa kama anahofu ya mungu.

“Ni muda sasa Spika atoke akiri amepokea taarifa ya wanachama wale kuvuliwa uanachama”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles