30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Bashungwa aagiza kuchukuliwa hatua wakandarasi wanaohatarisha maisha ya watanzania

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameziagiza Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kuhakikisha wanawachukulia hatua kali wakandarasi wanaohatarisha maisha ya watanzania kwa kujenga barabara zisizozingatia viwango na ambao leseni zao za uhandisi zimeisha kabla ya Marchi 31, 2024.

Pia amewataka wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi mbalimbali nchini kuzingatia taaluma yao na kuitumia vizuri ili kusaidia sekta hiyo ya ujenzi na nchi kukua kiuchumi.

Bashungwa ameyasema hayo leo Februari 26, 2024 wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya Mpango wa Mafunzo kwa Wahandisi Wahitimu (SEAP) wenye lengo la kuwajengea umahili wahandisi wanaomaliza vyuo vikuu, huku wahandisi zaidi ya 300 waliofuzu mafunzo hayo wakika kiapo umahili pamoja na uzinduzi wa mpango wa awamu ya tatu wa ufadhili huo kwa wahandisi wa kike katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema wanavyowajengea uwanja wa kucheza wasiaibishe nchi na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kalma yao ya uhandisi na ukandarasi.

“Tuanaamini kwa kufanya hivi kwanza utasaidia nchi kwa kuokoa fedha za kigeni na wakitengeneza nguvu ya taaluma hizi na kwa wale walio hitimu wanapaswa kuzingatia viapo,” amesema Bashungwa.

Amesema amezungumza na Benki ya Dunia miradi mikubwa ambayo inafadhiliwa na benki hiyo, katika kilometa 500 za barabara ambazo wamepata ufadhili wao, robo kilomita hizo watenge kwaajili ya wakandarasi wa ndani vigezo viendane na hao wakandarasi.

“Barabara zote ambazo zipo chini ya mitandao ya mkoani hadi sasa zipo kwa ajili ya wakandarasi wazawa pekee yao kwa maana ya fedha zipo mkoani ni soko la lisilopungua bilioni 550 hapo hazijawekwa za TARURA kwa mwaka ambazo ni takribani bilioni 229,” amesema.

Ameongeza kuwa wakijumlisha hapo wahandisi waliojaa kwenye ukumbi huo hizo fedha kwa ajili ya wakandarasi wazawa kwa upande wa malipo ya madeni serikali wanaendelea kujitahidi wasichukue muda mrefu ziwe zimelipwa.

Vilevile amesema Serikali inatambua juhudi za wahandisi kuleta maendeleo katika Taifa na wanafanyia kazi changamoto zinazokabili mradi wa SEAP.

Bashungwa amesema tukio hilo ni muhimu, mradi wa SEAP utasaidia kutatua changamoto ambazo wametaja na kuwakea misingi mizuri wahandisi.

Ametoa wito kwa wahandisi wote nchi kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa sababu wahandisi ni watu muhimu katika nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Khadija Khamis Rajabu pamoja na kupongeza ERB kwa mipango mbalimbali ya kusaidia vijana amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha sekta hiyo inaimarika .

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Wanandisi, Mhandisi Benard Kavishe amesema pamoja na sekta hiyo kuendelea kukua kwa Kasi upande wa wasichana idadi bado hairidhishi huku baadhi ya wadau kutoka Tarura, Tanroad, sekta binafsi na ILO nao wakiahidi kuendelea kuunga mkono mpango huo wa kuwajengea umahili wahandisi.

Amesema Bodi hiyo pia ipo mbioni kuanzisha shule ya taaluma hiyo ili kuwafikia vijana wanaohitimu wengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles