29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi wa Tanzania Algeria, Rais wa CAAID wateta

Na Mwandishi Wetu

BALOZI wa Tanzania nchini Algeria, Imani Njalikai amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu wa Afrika (CAAID), Dk. Amine Boutalbi katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano na CAAID ambayo ni kiungo muhimu kati ya ubalozi na sekta binafsi nchini Algeria katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Balozi Njalikai amesema ubalozi  huo utashirikiana na mamlaka za Tanzania  hasa  TPSF, TIC na Tantrade ili kufanikisha ushiriki wa wafanyabiashara kwenye makongamano ya uwekezaji na biashara yanayoandaliwa na CAAID, Mei 2024.

Balozi Njalikai ameongeza kuwa watashirikiana na  kituo hicho kuratibu kongamano maalumu la wafanyabishara wa Algeria nchini Tanzania mwaka 2024 kwa lengo kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya wafanyabiashara wan chi hizo mbili.

Naye Dk. Boutalbi amemhakikishia Balozi Njalikai  kuwa CAAID itaratibu ushiriki wa wafanyabiashara wa Algeria kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Saba Saba kwa mwaka 2024.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles