29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

TCAA kufunga mitambo mipya viwanja vya ndege

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepokea jumla ya makontena tisa yenye vifaa na mitambo ya kuongozea ndege ambavyo itafungwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizngumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari, amesema lengo la kufunga mitambo hiyo ni kuongeza ufanisi kwenye viwanja vya ndege.

Ametaja vifaa walivyopokea vilivyonunuliwa  na Serikali kutoka Norway na Italia kuwa ni radio za kidigital za masafa ya juu zinayojulikan kama VHF, mitambo ya kurekodi mifumo ya mawasiliano ya sauti(digital voice recording system) na mifumo ya kuunganisha ya kuangalia mawasiliano

“Nimpongeze Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha bilion 31.5 kwa ajili ya kuboresha mifumo ya mawasiliano kwenye viwanja vya ndege kati ya waongoza ndege na rubani,”amesema Johari.

Johari amesema mitambo hiyo itafungwa katika viwanja vya ndege na kwenye vituo 18 vya kurefusha na kukuza mawasiliano ya sauti, hivyo kuimarisha zaidi huduma za usafiri wa anga  na kuvutia  mashirika  kuja nchini.

“Tunachotarajia baada ya kufunga mitambo hii ni mawasiliano kati ya marubani na waongoza ndege katika anga lote la Tanzania na anga la juu la nchi ya Burundi yatakuwa yameborehwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa,”amesema Johari.

Amevita viwanja vitakavyofungwa mitambo hiyo kuwa  ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abeid Amani Karume Zanzibar, Songwe, Pemba, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dodoma Mtwara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Ametaja vituo hivyo ambavyo ni Kiuwe,Matogoro, Songea,Mbunga Mtwara,Mwasenyi ,Rufiji,Michakani Pemba,Arusha,Oldeianamalanja Ngorongoro,Kwejunga Tanga,Gairo Morogoro,Dodoma,Mwisi Tabora,kigoma,Nyamanya Bihalamuro,Mbiso Katavi,Kitulo,Muganza Butiama,Mara na Mugumu

Vituo vya mawasiliano ni Kiuwe, Matogoro, Songea, Mbunga Mtwara, Mwasenyi ,Rufiji, Michakani Pemba, Arusha, Oldeianamalanja Ngorongoro, Kwejunga Tanga,Gairo Morogoro, Dodoma, Mwisi Tabora, Kigoma, Nyamanya Bihalamuro, Mbiso Katavi, Kitulo, Muganza Butiama, Mara na Mugumu

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Frola Mwanshinga amesema mifumo hiyo itafanya kazi kwa pamoja na nchi jirani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles