22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Bado kuna upungufu wa Wahandisi Wanawake- Kumbilamoto

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Jiji la Dar es Salaam limekiri kuwa kuna upungufu mkubwa wa Wahandisi Wanawake unaochangia kuongeza changamoto katika sekta hiyo nchini, hali inayosababisha waliopo pia wasiwe na uwezo wa kupigania changamoto zinazoikumba fani hiyo.

Akizungumza na wakati akifungua Kongamano la Mtandao wa Wanawake katika sekta ya Nishati Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, ambalo lilikutanisha Wanawake kwa ajili ya kujadili changamoto zao. Amesema serikali inaongeza ufadhili katika masomo hayo hasa kwa wanafunzi wa kike ili kuleta uwiano sawa katika sekta ya nishati na masomo ya Sayansi kwa ujumla.

“Upungufu mkubwa wa Wahandisi wanawake unaochangia kuongeza changamoto katika sekta ya hii nchini, hali inayosababisha waliopo pia wasiwe na uwezo wa kupigania changamoto zinazoikumba sekta hii.

“Niwakati wa wanawake kujituma ili kuondoa changamoto hizi katika sekta ya uhandisi na kuwasaidia wengine kuona thamani ya mnachokifanya,” amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wake, Mhandisi Juliana Pallangyo ambaye pia amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, amesema wanawake wahandisi wana uwezo sawa na Wanaume katika utendaji hivyo waongezewe nguvu.

“Wanawake wakiongezewa nguvu ya kupewa nafasi na uwezeshwaji kimitaji watafanya mambo makubwa zaidi ya wanaume katika fani ya uhandisi,”Mhandisi Juliana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles