24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Baa la njaa lamtisha mbunge

joel-mwaka_210_120NA RAMADHAN HASSAN, CHAMWINO

MBUNGE wa   Chilonwa, Joel Mwaka (CCM) amemwomba Waziri Mkuu   kuwasaidia chakula wakazi wa jimbo lake  ambao sehemu kubwa wamekumbwa na baa la njaa.

Aliyasema hayo  katika ziara yake ya kukagua hali ya mimea katika vijiji vya Dabalo na Majeleko  wilayani hapa.

Mwaka  alisema chakula walichopewa awamu ya kwanza hakitoshi na hivi sasa wananchi  wanalazimika kuvuna mazao ambayo hajakomaa ili wafanye chakula.

“Ninamuomba sana mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa  awasaidia wananchi wa jimbo langu waweze kuepukana na baa la njaa ambalo   linaendelea kuwatesa.

“Nimefanya kila aina ya jihihada lakini hali inazidi kuwa mbya imefika mahali mahindi ambayo bado hayajakomaa yanavunwa na wananchi na kuyafanya chakula.

“Kama hali itaendelea kuwa hivi huko tuendako huenda kukawa na balaa zaidi kwa vile  mahindi hayana hata watoto lakini yanavunwa, hii ni hatari sana,” alisema Mbunge Mwaka.

Pia Mbunge huyo alitimiza ahadi yake ya kuwapatia wakazi wa jimbo hilo maji safi na salama kwa kupeleka wataalamu kuchimba kisima katika Kijiji cha Dabalo.

“Nadhani mnawaona watu kutoka wizarani wakipima ni eneo gani tunaweza kupata maji niwahakikishie ile ahadi yangu wakati wa kampeni sasa ninaitimiza kwa kuwaletea maji safi na salama,’’ alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles