26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kikwete afichua siri za ushindi wa CCM katika uchaguzi

kikweteNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amefichua mbinu za chama hicho kushinda uchaguzi mbalimbali ukiwamo uchaguzi Mkuu.

Kikwete alifichua moja ya mbinu hizo jana kwenye kumbukumbu ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na mwimbaji maarufu wa CCM, marehemu Kapteni John Komba.

Alisema Komba alikuwa   mtu wa aina yake kwa kuwatumia wasanii mbalimbali wa muziki na mwenye ushawishi kwa wapiga kura.

“Wapo wapiga kura ambao walitupigia kura baada ya kuona msanii wanayempenda amepanda jukwaani kwetu kutumbuiza.

“Hali hiyo iliwafanya kutupigia kura kwa sababu wamemuona msanii wanayempenda anatukubali,” alisema Kikwete.

Alisema kwa kutumia mbinu hiyo na nyingine CCM ilijikuta ikiendelea kuwaangusha wapinzani   kila uchaguzi unapotokea.

“Wapinzani wamekuwa wakijitahidi kutuangusha lakini wanashindwa kutokana na mbinu zao kuwa dhaifu, mwisho wanajikuta wakiishia kukasirika,” alisema Kikwete.

Mwenyekiti huyo wa CCM akimzungumzia Komba, alisema alikuwa rafiki yake mkubwa tangu wakiwa jeshini na alikuwa mchango mkubwa kwa CCM.

Kikwete   alitumia fursa hiyo kuzindua kitabu cha historia ya Marehemu Komba kilichoandikwa na mwandishi Yusuph Halimoja, kikijulikana kama ‘Maisha ya Mzalendo’.

Lengo la mauzo ya kitabu hicho ni kusaidia kupatikana   Sh milioni 200.

“Naamini Watanzania hawana utaratibu wa kusoma ila kutokana na ukaribu wangu na marehemu, nitasaidia kutafuta fedha nyingine kwa kuandaa harambee ili shule   iweze kujengwa,” alisema Kikwete.

Kikwete alisema   atahakikisha anasimama pamoja na familia hiyo ya marehemu Komba kujenga shule hiyo inayotarajiwa kujulikana kama John Komba Primary & Secondary School itakayojengwa   Kiromo, Bagamoyo.

Alisema kiwanja hicho kilinunuliwa kutokana na malipo ya nyimbo  za mwisho za marehemu  Komba, ambayo alikuwa akiidai CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles