MBUNGE wa Chilonwa, Joel Mwaka (CCM) amemwomba Waziri Mkuu kuwasaidia chakula wakazi wa jimbo lake ambao sehemu kubwa wamekumbwa na baa la njaa.
Aliyasema hayo katika ziara yake ya kukagua hali ya mimea katika vijiji vya Dabalo na Majeleko wilayani hapa.
Mwaka alisema chakula walichopewa awamu ya kwanza hakitoshi na hivi sasa wananchi wanalazimika kuvuna mazao ambayo hajakomaa ili wafanye chakula.
“Ninamuomba sana mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa awasaidia wananchi wa jimbo langu waweze kuepukana na baa la njaa ambalo linaendelea kuwatesa.
“Nimefanya kila aina ya jihihada lakini hali inazidi kuwa mbya imefika mahali mahindi ambayo bado hayajakomaa yanavunwa na wananchi na kuyafanya chakula.
“Kama hali itaendelea kuwa hivi huko tuendako huenda kukawa na balaa zaidi kwa vile mahindi hayana hata watoto lakini yanavunwa, hii ni hatari sana,” alisema Mbunge Mwaka.
Pia Mbunge huyo alitimiza ahadi yake ya kuwapatia wakazi wa jimbo hilo maji safi na salama kwa kupeleka wataalamu kuchimba kisima katika Kijiji cha Dabalo.
“Nadhani mnawaona watu kutoka wizarani wakipima ni eneo gani tunaweza kupata maji niwahakikishie ile ahadi yangu wakati wa kampeni sasa ninaitimiza kwa kuwaletea maji safi na salama,’’ alisema