24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Azam, Power Studio wazindua filamu ya EONII

Na Esther Mnyik, Mtanzania Digital

Kampuni ya Azam Media kwa ushirikiano na Power Studio wamezindua filamu ya kwanza yenye ubunifu wa Kisayansi na elimu ya sayansi itakayomfanya mtazamaji kutazama na kujifunza.

Akizungunza Mei 29, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Yahaya Mohamed amesema ni filamu ya kwanza ya kisayansi kufanywa hapa nchini ikiwa inalenga kuonyesha vipaji na uwezo mkubwa ndani ya tasnia ya filamu.

“Kama taasisi tukiwa na maono ya kuimarisha tasnia ya filamu ya Tanzania katika soko la kimataifa, Azam Media na Power Brush Studio tumeshirikiana kutengeneza filamu kwa kutumia timu ya utayarishaji wa ndani yenye ujuzi inaonyesha simulizi wa hadithi na utaalamu wa kiufundi katoka tasnia ya filamu Tanzania na kutoa vipaji,” amesema Yahya.

Amesema filamu hiyo ijulikanayo kwa jina la “EONII” imezinduliwa na itaonyeshwa katoka kumbi za filamu maarufu kama Theatre hivi karibuni katika mikoa mitano.

Ametaja mikoa hiyo ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga na kwa upande wa Zanzibar itaonyeshwa kwenye Tamasha la Ziff ikiwa ni njia mojawapo wapo ya kukuza utalii nchini.

“EONII filamu imebeba hadithi ya kuvutia ugunduzi wa kisayansi katika uhitaji wa nishati ya uhakika na kukosekana kwake kunakozua taharuki katika jamii husika madoido ukisasa unaotumika kuzungumzia mkasa huu itabaki kama alama ya furaha mioyoni mwa Watanzania wengi wapenzi wa filamu,” ameongeza Mohamedi.

Naye Mkurugenzi wa Studio za Power Brush, Eddie Mzale amesema kuwa wamewekeza ubunifu na maarifa katika kuandaa filamu hiyo.

“Tunajivunia sana kwa namna filamu hii ilivyotoka kuanzia ubora mpaka hadithi yenyewe hivyo tunaamini filamu hii siyo tu inavutia watazamaji ulimwengu kote lakini pia kama chachu ya ukuaji wa tasnia ya filamu ya Tanzania,” amesema Mzale.

Aidha, amesema kuwa filamu hiyo imetumia miaka sita hadi kukamilika kwake hivyo ametoa rai kwa wasanii wa filamu kujiamini na kutokukata tamaa kwenye kazi zao kwani kiu ya Serikali ya Tanzania na Wizara husika ni kuona wasanii wanapiga hatua katika filamu zao Kimataifa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles