21.9 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Aussems: Nahitaji pointi tatu tu

MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

ILI kuhakikisha wanafanya vizuri na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema kwanza anahitaji pointi tatu muhimu katika mechi dhidi ya Mbao FC, katika mchezo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa  Jamhuri, mjini Morogoro.

Baada ya mchezo huo, Aprili 6 wataanzia nyumbani dhidi ya Mazembe katika mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana, mara baada ya mazoezi, Aussems alisema kwa sasa akili na nguvu zao wanazielekeza katika mechi dhidi ya Mbao, kutokana na kuhakikisha wanapata pointi muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa.

Alisema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika kila michuano iliyokuwa karibu yao, kutokana na mechi ya Mbao kuwa karibu, sasa akili zake ni kuhakikisha wanapata pointi muhimu ili kumuweka katika mazingira mazuri katika mbio za ubingwa.

“Tulipoteza mechi ya kwanza na Mbao Mwanza na sasa tumejipanga kuchukua pointi hizo tatu na kuhakikisha tunaanza kuutumia vyema uwanja wetu wa Jamhuri ambao tunaanza nao katika mchezo huu.

“Kutumia Uwanja wa Jamhuri kama nyumbani hatuna jinsi, kutokana na tayari umefungiwa, kwani ukiangalia kuna tofauti kubwa na Uwanja wa Taifa upo vizuri,” alisema Aussems.

Kikosi cha Simba jana kiliendelea na mazoezi  katika Uwanja wa Boko Veteran kikiwa na wachezaji wachache, huku wengine wakiitwa katika timu za Taifa, wanatarajia kujiunga leo na kesho kuingia kambini Sea Scape.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,717FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles