25.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

Aubameyang: Makubwa yanakuja Dortmund

Pierre-Emerick Aubameyang
Pierre-Emerick Aubameyang

DORTMUND, UJERUMANI

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa makubwa yanakuja msimu huu.

Nyota huyo ambaye alifanya vizuri msimu uliopita kwa kupachika mabao mengi ndani ya klabu hiyo katika mchezo wake wa kwanza msimu huu ambao ulipigwa juzi, nyota huyo aliifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mainz.

Aubameyang raia wa nchini Gabon, msimu uliopita alitwaa uchezaji bora barani Afrika, hivyo mchezaji huyo amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kusubiri makubwa yanakuja msimu huu.

Msimu uliopita mchezaji huyo alifunga mabao 25 katika Ligi ya nchini Ujerumani huku akiwa nyuma ya nyota wa Bayern Munich, Roberto Lewandowski ambaye alifunga mabao 30.

Nyota hao wawili wameonekana kuwa na upinzani mkubwa msimu uliopita na hata msimu huu wanaonekana kuwa watakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Lewandowski mchezo wake wa kwanza amepachika mabao matatu, huku Aubameyang akifunga mabao mawili.

“Msimu umeanza, nashukuru nimeanza kwa kufunga mabao mawili, ninaamini msimu huu utakuwa wa mafanikio kutokana na maandalizi yaliyofanyika.

“Msimu uliopita nilifanya vizuri kutokana na ushirikiano na wachezaji wenzangu, hivyo ninaamini hata msimu huu ninaweza kufanya zaidi ya msimu uliopita, hivyo mashabiki wa Dortmund wakae tayari makubwa yanakuja.

“Kila siku nawaza nini mashabiki wangu wanakitaka, lakini jibu langu ni moja tu kwamba wanataka kuiona timu yao ikifanya vizuri, hicho ndicho ninachotaka kukifanya kuisaidia timu,” alisema Aubameyang.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles