32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

ASKARI 14 WATAJWA BIASHARA DAWA ZA KULEVYA

Na Muhammed Khamis (UoI) – ZANZIBAR


ASKARI 14 wa Jeshi la Polisi Zanzibar wanatuhumiwa kushirikiana na waingizaji wa dawa za kulevya visiwani Zanzibar

Akitoa taarifa mbele ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya, Rogers Siyanga, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud, alisema hivi sasa wameshakamilisha utaratibu wa kuwafikisha askari hao katika vyombo vya sheria.

Alisema hatua hiyo inatokana na agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli, la kupiga vita uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya nchini.

“Kila mmoja wetu anapaswa kutambua madhara ya utumiaji wa dawa za kulevya ambazo kwa sasa zimekuwa zikiathiri kundi kubwa la vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

“Kutokana na hali hiyo, tayari tumeimarisha ulinzi katika sehemu mbalimbali za mkoa wetu, ikiwamo pia katika bandari bubu na uwanja wa ndege ambako ulinzi umeimarishwa,” alisema Ayoub.

Aidha aisema hivi karibuni watu wanaofanya biashara hiyo kwa kushirikiana na watumishi wa Serikali ambao si waaminifu, walimuua mbwa aliyekuwa akifanya ukaguzi katika mizigo Uwanja wa Ndege.

Kwa upande wake Kamishna Siyanga alisema kuwa suala la mapambano dhidi ya dawa za kulevya si vita ya Dar es Salaam pekee ila ni ya Tanzania nzima, ikiwamo Zanzibar.

“Ninachoomba wananchi waendelee kutoa taarifa na ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuweza kudhibiti dawa za kulevya. Jamii bora itajengwa na Watanzania wote tuendelee kushirikiana ili kuijenga nchi yetu bila dawa za kulevya,” alisema Siyanga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles